Hungary yawa macho na mbinu za wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wahamiaji wanaoingia nchi za Ulaya

Serikali ya Hungary imeendelea na msimamo wake dhidi ya wahamiaji wanaotaka kutumia reli kuu ya nchi hiyo, kuvuka kuelekea mji mkuu wa taifa hilo Budapest, na hatimaye kuingia nchi za mataifa ya Ulaya.

Watu walio wengi walikuwa wakizuiwa kupanda treni ili kutotumia mwanya huo kuingia Austria na Ujerumani.

Msemaji wa serikali ya Zoltan Kovacs anasema kuwa kinachopaswa ni kufanyia marekebisho sheria.

Ameitaja Ugiriki, kuwa ni moja ya mataifa yanayotoa mwanya kwa maelfu ya wahamiaji wanaoingia Ulaya bila ya kuwa na aina yoyote ya usajili.

Inakadiriwa wahamiaji wapatao 240,000 wamefika Ugiriki kupitia mfumo huo.