Al Shabaab yashambulia kambi ya AMISOM

Image caption Wapiganaji wa Al Shabaab

Taarifa kutoka Somalia zinasema kuwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab limeshambulia kambi ya kikosi cha walinda usalama wa muungano wa Afrika AMISOM.

Wengi wamejeruhiwa katika shambulio hilo wakiwemo wanajeshi hao wa AMISOM.

Al-Shabaab wamejisifia kuwa mmoja wa walipuajI wake wa kujitolea ameliendesha gari liliolkuwa na bomu ndani yakambi ya Janale, yapata kilomita tisini kutoka mji mkuu Mogadishu kisha wapiganaji wake wengine wakashambulia kwa risasi.

Kwa mujibu wa Al shabaab, wanajeshi hamsini wa AMISOM wameuawa japo ripoti hizo hazijathibitishwa kutoka upande wa AMISOM.

Waandishi wametahadharisha kuwa wapiganaji hao wamekuwa wakizidisha chumvi kwa taarifa wanazotoa juu ya mashambulio wanayofanya.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Jengo lililoshambuliwa na Al shabaab mjini Mogadishu