Sheria mpya yaanza kutumika TZ licha ya upinzani

Haki miliki ya picha
Image caption Ramani ya Tanzania

Leo ni mwanzo wa kutumika kwa sheria ya makosa ya mtandaoni iliyoleta mzozo nchini Tanzania.

Kuambatana na sheria hiyo kusambaza taarifa zisizo sahihi, zenye kupotosha unaweza kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha jela au kulipa faini.

Kumekuwepo na upinzani mkubwa kutoka kwa vyombo vya habari na wamiliki wa mitandao ya kijamii kuhusiana na sheria hiyo.

Moja kati ya malalamiko juu ya sheria hii ya mitandao ya mwaka 2015 ni mamlaka inayowapatia wasimamizi wa sheria hii.

Polisi wana mamlaka ya kuchukua na kukagua simu, kompyuta na kukagua taarifa mbalimbali katika vifaa binafsi vya mawasiliano bila waranti.

Sheria hiyo pia inawataka watoa huduma za simu kukabidhi taarifa za wateja wao kwa mamlaka.

Serikali inasema sheria hiyo inahitajika kwa kuzuia matumizi mabaya ya mitandao na kulinda makundi mbalimbali kama watoto.

Tangu kuanzishwa kwa mkongo wa mawasiliano, jamii ya watanzania mitandaoni imezidi kuongezeka kwa mfano watumiaji wa mitandao ya kijamii kama whatsapp kwenye simu za mkononi.

Wanaharakati wanasema wataendelea kupinga maeneo kadhaa kandamizi katika sheria hiyo.