Segun Odegbami ajitosa Urais Fifa

Image caption Segun Odegbami anawania Urais wa FIFA

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria Segun Odegbami ametangaza nia ya kuwania kiti cha urais katika chama cha soka duniani FIFA.

Segun mwenye miaka 63 Alitwaa kombe la mataifa ya Afrika mwaka 1980 aikwa mchezaji wa kikosi cha Nigeria Super Eagle.

Anakuwa mwaafrika wa pili kutangaza nia ya kuwania cheo hicho kikubwa katika shirikisho hilo la mpira baada ya Musa Bility, wa Libery kutangaza kuwa atapigania nafasi hiyo.

Uchaguzi wa Fifa unatarajiwa kufanyika Februari 26, 2016, tayari Rais wa chama cha soka cha ulaya Michael Platin ameonyesha nia ya kutaka nafasi hiyo sambamba na Mong-joon wa Korea kusini

Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Zico na David Nakhid toka visiwa vya Trinidad na Tobago nao wameshatangaza nia.