Uchina yakumbuka ushindi dhidi ya Japan

Haki miliki ya picha
Image caption Gwaride la ushindi lafana China

Nchini Uchina, Rais Xi Jinping, ameshuhudia gwaride maalum la ushindi kuadhimisha miaka 70 tangu taifa hilo lilipoishinda Japan katika mapambano.

Gwaride hilo pia limewahusisha wapiganaji wa zamani wa vita vya pili vya dunia ambao walionekana wakipunga mikono kuwasalimia watu waliokuwa wanashuhudia tukio hilo.

Katika hotuba ya ufunguzi ya rais Xi Jinping, alitoa salamu za kipekee kwa wale waliopigana vita na kufanikiwa kuiangusha Japan.

Wakati wa gwaride hilo vifaa mbalimbali vya kijeshi vilionyeshwa ziwemo silaha za kivita.