Mjadala mkali kuhusu wahamiaji EU

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji wakiwa safarini kwenda Ulaya

Tatizo la wahamiaji imekuwa agenda kuu na kuzusha mjadala mkali katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa muungano wa ulaya mjini Luxermbourg.

Waziri wa Mambo ya nje ya Hungary Peter Szijjarto amesema matukio ya hivi karibuni katika nchi yake ni matokeo ya kile alichokiita kushindwa kwa sera ya uhamiaji katika nchi za ulaya.

Naye waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Austria Sebastian Kurz amesema mgogoro wa wahamiaji umeamsha wito kwa Ulaya na za Muungano wa nchi za Ulaya EU kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maelfu ya wahamiaji wameamua kutembea kwa miguu

Ujerumani ikiwa inaungwa mkono na tume ya ulaya imekuwa ikitaka nchi za Ulaya zigawane wakimbizi na wahamiaji.

Lakini suala hilo limepingwa na nchi nyingi kutoka mashariki mwa Ulaya.