Chanzo cha wakimbizi kishughulikiwe

Msukosuko wa wakimbizi Haki miliki ya picha Daniel Etter NY Times Redux eyevine

Waziri wa fedha wa Uingereza, George Osborne, ambaye amekuwa akikutana na mawaziri wa fedha wengine katika mkutano wa nchi 20 tajiri kabisa duniani, yaani G20, Ankara, Uturuki, anasema nchi lazima ziwape hifadhi watu wanaokimbia adhabu.

Lakini alisema piya inafaa kuwa na "mpango kamili" wa kupambana na watu wanaosafirisha watu kimagendo, na kumaliza vita vya Syria:

"Ni lazima tuyashinde haya magengi ya wahalifu wanaosafirisha watu kimagendo na wanaohatarisha maisha ya watu na kuuwa watu.

Tena bila ya shaka lazima tushughulike na tatizo kwenye chanzo, ambacho ni hii serikali ovu ya Assad na magaidi wa ISIL; na unahitaji mpango kamili wa kurejesha amani na utulivu nchini Syria.

Ni kazi kubwa bila ya shaka, lakini hatuwezi kuacha msukosuko huu kutokota tu; ni lazima tuushughulikie.

Kwa hivyo kuna mambo mengi tunahitaji kufanya, na yakifanywa yote ndio tutapata ufumbuzi wa hii changamoto kubwa sana."