Mafuta kuporomoka yaumiza Saudi Arabia

Machimbo ya mafuta Saudi Arabia Haki miliki ya picha

Serikali ya Saudi Arabia inapanga kupunguza matumizi kwa sababu ya bei ya mafuta kuporomoka - pato kubwa la nchi hiyo linatokana na kuuza mafuta nchi za nje.

Waziri wa Fedha, Ibrahim Alassaf, alisema baadhi ya miradi iliyokuwa imepitishwa, sasa huenda ikaahirishwa.

Hakutoa maelezo zaidi lakini alisema bajeti ya sekta muhimu kama afya na elimu haitoathirika.

Serikali ya Saudi Arabia imetabiri nakisi katika bajeti ya mwaka huu ya karibu dola bilioni 40, lakini wadadisi wa kimataifa wanafikiri huenda ikawa kubwa zaidi.