Rais Buhari asifia jeshi lake

Image caption Rais Buhari

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amesema kikosi chake cha ulinzi kimepata mafanikio katika mapambano yake dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram.

Katika mahojiano na BBC, Rais Buhari amesema malengo yake ni kuona kwamba wapiganaji hao wa kiislamu hawajiimarishi na kuteka miji na vijiji.

Mwezi uliopita Buhari aliahidi kuwashinda wanamgambo hao wa Boko Haram ndani ya miezi mitatu.

Amefahamisha pia kwamba kundi la watu lililotekwa na Boko Haram katika msitu wa Sambisa limegunduliwa lakini bado haijafahamika wazi kama kati ya hao ni wanafunzi wa kike waliotekwa kutoka Chibok mwaka uliopita.