Mama Mpalestina aliyechomwa aaga dunia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mtoto wake wa miezi 18 aliuawa katika shambulio hilo pamoja na mumewe ambaye alikufa hospitalini wiki moja baadaye .

Mwanamke mmoja wa kipalestina amekufa kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa shambulio mwezi Julai lililomuua mumewe na mtoto wao mdogo wa kiume.

Riham Dawabsha alikua anauguza majeraha ya kuungua kiasi cha asilimia tisini ya mwili wake aliyoyapata baada ya nyumba yao kupigwa na mabomu ya moto katika kijiji cha Duma kilichopo katika ukingo wa magharibi .

Shambulio hilo linaaminiwa kufanywa na walowezi wa kiyahudi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mama Mpalestina aliyechomwa aaga dunia

Mtoto wake wa miezi 18 aliuawa katika shambulio hilo pamoja na mumewe ambaye alikufa hospitalini wiki moja baadaye .

Mtoto mwingine wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne bado anapata matibabu ya majeraha.

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Shambulio hilo lililaaniwa na jamii ya kimataifa

Shambulio hilo lililaaniwa na jamii ya kimataifa na kusababisha maandamano makubwa ya wapalestina

Maafisa wa polisi nchini Israeli waliwakamata watu 7 wanaoshukiwa kuvamia nyumba hiyo ya mpalestina katika ukingo wa magharibi na kuiteketeza moto.