Ujerumani na ongezeko la wahamiaji

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Polisi wa Ujerumani akizungumza na wahamiaji

Serikali ya Ujerumani imetangaza hatua kadhaa zitakazotumiwa kuisaidia kukabiliana na ongezeko la wahamiaji

Miongoni mwa hatua hizo, ni kutoa kiasi cha fedha dola bilioni tatu kusaidia serikali za majimbo na manispaa.

Pia imeamua kuharakisha mchakato wa kupitia maombi ya wanaotaka hifadhi, kutoa nyumba na kutenga fedha kwa ajili ya kulipa marupurupu kwa wageni.

Tangazo hilo limetolewa baada ya mkutano wa uliodumu kwa saa tano baina ya chansela, Angela Merkel, na washirika wake.

Takriban wahamiaji wapatao elfu kumi na nane wanakadiriwa kuingia nchini Uingereza mwisho mwa juma kufuatia makubaliano na Austria na Hungary kulegeza sheria za wanaoomba hifadhi.