Utafiti kuchunguza jinsi mtu anavyozeeka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Vipimo mbalimbali pia huchukuliwa

Wanasayansi mjini London wamegundua utafiti mpya wa kuchunguza utaratibu wa jinsi mtu anavyo zeeka.

Unaangalia tabia ya zaidi mamia ya vinasaba vya damu, ubongo na seli za misuli.

Wanasayansi hao wameambatanaisha matokeo ya watu wenye afya nzuri walio na umri wa miaka 63 na zile za vijana kutengeneza mpagilio wa kufuatilia ili kuweza kuzeeka kwa afya zaidi.

Wanasayansi hao pia wamegundua katika baadhi ya kesi, watu huzeeka kwa zaidi ya miaka 15 na umri wao halisi. Wanasema urafiti huo utasiaidia kugundua watu walio kwenye hatari ya kupata magonjwa.