Migodi ya shaba kufungwa Zambia na Congo

Haki miliki ya picha afp
Image caption Migodi ya shaba kufungwa Zambia na Congo

Taarifa kutoka kwa kampuni kubwa ya uchimba ugodi Glencore imesema kuwa imesitisha uzalishaji wa madini ya shaba katika nchi ya jamhuru ya kidemokrasia ya Congo na Zambia.

Hatua hii imesababisha mtikiso mkubwa katika mataifa hayo mawili .

Aidha wasiwasi umeongezeka kuhusuiana na ukosefu wa kazi.

Mwaandishi wa BBC Mattew Davies amesema hatua ya Glenmore itaathiri takriban robo ya uzalishaji wa shaba katika nchi ya demokrasia ya Congo na Zambia.

Haki miliki ya picha
Image caption Kupunguka kwa kasi ya ukuaji nchini China kumesababisha kushuka kwa mahitaji ya shaba .

Afrika ni wazalishaji wa pili wa vyuma.

Zambia hutegemea asilimia sabini ya mauzo ya nje ya madini ya shaba.

Kampuni hiyo imesema itasitisha uzalishaji katika sehemu ya Mopani, Zambia na Katanga DRC kwa zaidi ya miezi kumi na nane.

Kusitishwa kwa uzalishaji kutapunguza uzalishaji wa tani elfu mia nne itakayosababisha mfumuko wa bei ya shaba.

Kwa hivi sasa uzalishaji umepungua kwa asilimia 40 .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Zambia hutegemea asilimia sabini ya mauzo ya nje ya madini ya shaba.

Mbali na ukosefu wa kazi, hatua hii pia itapunguza mapato ya kodi na zao la nchi.

Uamuzi wa Glenccore unaweza kusababisha kampuni zingine za ushalishaji wa shaba kufuatwa mkondo huo.

Mgogoro huu umesababishwa maelfu ya maili kutoka Afrika nchini China, ambapo kupunguza kasi ya ukuaji kumesababisha kushuka kwa mahitaji ya shaba .