Papa Francis kurahisisha sheria ya talaka

Haki miliki ya picha AP
Image caption Papa Francis kurahisisha sheria ya talaka miongoni mwa wakatoliki

Papa Francis anatarajia kurahisisha taratibu zinazoruhusu wafuasi wa kanisa katoliki waliooana kutoa talaka na kuolewa tena huku wakibakia kuwa wafuasi wa katika kanisa hilo .

Maelezo ya taratibu hizo yanatarajiwa kutangazwa mjini Vatcan baadaye leo .

Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa mbinu ya kurekebisha taratibu hizo zinazoruhusu wanandoa kuachana na kupunguza gharama .

Haki miliki ya picha ap
Image caption Papa aliunda tume ya wanasheria wa kanisa mwaka jana kupiga msasa

Bila sheria hiyo wanandoa wa kikatoliki wanaotalikiana na kuolewa upya hutazamwa kama wazinifu na hawaruhusiwi kupokea komunio.

Mwandishi wa BBC mjini Vatican anasema kuwa Papa Francis hatabadilisha mafunzo ya katoliki kuhusu kuachana kwa wanandoa , lakini atawezesha kurahisisha wanandoa wenye matatizo kuthibitisha kuwa ndoa yao haikuwa ya maana tangu mwanzo