Wahamiaji wachanja mbuga kuelekea Ulaya

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wahamiaji wakielekea Ulaya

Maelfu ya Wahamiaji wanajaribu kuingia bara Ulaya.

Huku Umoja wa Ulaya ukiangalia uwezekano wa kuwashughulikia wale ambao tayari wapo huko.

Shirika la Umoja wa Mataifa la huduma kwa Wakimbizi limeanza kuwasaidia maafisa wa Ugiriki kuwapokea idadi kubwa ya wahamiaji wapya wanaowasili katika kisiwa cha Lesbos.

nchini Hungary nako, mamia ya wahamiaji walipita kwenye mistari ya polisi kwa nguvu na kuvuka mpaka wa kuingia Serbia.

Wito wa Ufaransa na Ujerumani wa kuwekwa kwa mifumo ya kisheria ya kugawana wakimbizi baina ya wanachama wa Muungano wa Ulaya umepingwa na serikali kadhaa.