Rais wa Zamani wa Guatamala kushtakiwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa zamani wa Guatamala Otto Perez Molina

Jaji nchini Guatemala ameamuru rais wa zamani wa nchi hiyo Otto Perez Molina,kufika mahakamani kukabiliana na mashtaka ya ufisadi kufuatia sakata ambayo ilisababisha miezi kadhaa ya maandamano.

Bwana Perez Molina, ambaye alijiuzulu wiki iliyopita amekana kufanya kosa lolote.

Mwendesha mashtaka aliandaa ushahidi wake kwa kuzingatia ushahidi maelfu ya mawasiliano ya simu.

Viongozi wakubwa wengi wa kisiasa wamehusika katika kashfa hiyo.

Image caption Maandamano yaliyopelekea rais Otto Perez Molina kujiuzulu

Bunge la nchini Guatemala limemwapisha makamu wa rais Alehandro Maldonado, mpaka rais mpya atakapo chukua madaraka hayo mwezi januari.

Muigizaji wa vichekesho, Jimmy Morales, alishinda kura nyingi katika uchaguzi siku ya Jumapili lakini hazikutosha ili kuepuka kurudiwa kwa mwezi ujao.