Nato yasikitishwa Urusi kuisaidia Syria

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Rais wa Syira Bashar Al assad

Mkuu wa Nato anasema amesikitishwa kuhusu taarifa kuwa Urusi ina mpango kuongeza uwepo wake wa kijeshi nchini Syria.

Jens Stoltenberg amesema kuwa hiyo haitasaidia kupunguza mzozo uliopo hivi sasa.

Katika wiki za karibuni ,kumekuwa na dalili kuwa Urusi inaweza kuimarisha mchango wake nchini Syria.Pamoja na Iran, Urusi imekuwa msaidizi muhimu ya Rais Assad.

Maafisa wa marekani wamewaambia waandishi wa habari kuwa Moscow imetuma ndege mbili za nyongeza kwenda Syria siku mbili ama zaidi zilizopita.Msemaji wa wizara ya kigeni ya Urusi amedhibitisha kuwepo kwa vikosi vya usalama nchini Syria,lakiai akasema hakukua na kipya zaidi ya kulinda amani.