Nigeria kufunga baadhi ya balozi zake

Image caption Rais Muhammadu Buhari amesema huenda akafunga balozi zake ilikupunguza matumizi ya fedha

Nigeria inazingatia kufunga baadhi ya ofisi za balozi wake wa kigeni ili kupunguza gharama.

Rais mpya Muhammadu Buhari ametangaza kuwa kuwepo kwa balozi za taifa hilo katika mataifa mengi ya kigeni kuna gharama na pesa kwa sasa hazipo.

Katika ujumbe kwa vyombo vya habari Buhari amesema ,

‘ hakuna haja ya kuweka balozi ambazo hazina vifaa vya kutosha na wafanyikazi wasiokuwa na motisha kazini’

Image caption Buhari ;hakuna haja ya kuweka balozi ambazo hazina vifaa vya kutosha na wafanyikazi wasiokuwa na motisha kazini

Taarifa hii imenukuliwa wakati rais huyo alipokuwa akiwahutubia viongozi wa maswala ya kigeni.

‘Tujaribu kufanya kile tunachoweza , kwa sasa hatuwezi kufanya mengi na hakuna haja ya kujifanya .’alisema Buhari.