Safari za treni kuanza tena Denmark

Image caption wahamijaji

Usafiri wa treni nchini Denmark umejea tena baada ya hapo kusitishwa kwenda na kutoka Ujerumani baada ya kutokuelewana kati ya polisi na mamia ya wahamiaji.

Kundi moja la wahamiaji lilikataa kushuka katika treni waliyokuwemo kwa madai ya kutaka kusafiri kwenda Sweden ambayo ina sheria nzuri ya uhamiaji kushinda Denmark.

Polisi wamekuwa wakiwazuia mamia wengine wa wahamiaji waliokuwa wakitembea kwa miguu nchini Denmark kwa lengo la kufika Sweden.

Taarifa zinasema kuwa baadhi ya wahamiaji wamekuwa wakiwahadaa polisi kwa kujificha katika magari ama katika matrekta yanayokokotwa na farasi.