Majaji wa mahakama wadaiwa kula hongo

Haki miliki ya picha ap
Image caption Jaji

Tuelekee Ghana sasa ambako nchi hiyo imeanza kuchunguza tuhuma za rushwa dhidi ya majaji zaidi ya 30 katika mahakama ndogo na kubwa nchini.

Majaji hao ni sehemu ya maafisa wengine 180 wa mahakama waliotuhumiwa katika uchunguzi wa miaka miwili na mwandishi mashuhuri nchini humo, Anas Aremeyaw Anas.

Mwandishi huyo anasema ana nakala za video za majaji hao wakituhumiwa kupokea na kuitisha mlungula kutoka kwa washtakiwa.

Kamati ya leo imekua ikisikiliza kauli za majaji waliotuhumiwa.

Majaji 22 kutoka mahakama za chini wamefika mbele ya kamati kuijitetea.

Wengi hawafahamu jinsi ya kujibu madai dhidi yao.

Lakini kwa sasa majaji hawa wameachishwa kazi hadi uchunguzi dhidi yao kufanyika.

Pia kwenye kamati hii wamefika majaji wa mahakama kuu, ambapo wamepewa hadi leo kujibu tuhuma dhidi yao.

Duru zinasema wmeonyeshwa kanda zilizowanasa kwa mara ya kwanza, na hijulikani ikiwa wamejibu kuhusu hilo.

Vikao vya kamati hii vinafanyika faraghani na ni taarifa finyu sana ambazo zimewekwa kwa raia.

Idara ya mahakama imesema itatoa taarifa baada ya uchunguzi kukamilika..

Mmoja wa watunga filamu Anas Aremeyaw anasema walikwenda kwa majaji hao na kuwahonga ili kuwaachia washukiwa baadhi wakiwa ni wezi wa mabavu.

Ni taarifa ambazo zimevutia mjadala wa umma nchini Ghana.

Japo wengi hawajashangazwa, wamesema hii inadhihirisha imani yao kwamba rushwa imekua ikiendelea katika mahakama.

Kwa sasa kumezuka mjadala ikiwa Bw Anas anafaa kuweka kanda hii hadharani au la.

Baadhi wanaunga mkono hilo lakini wengi wanasema huenda ikaharibu sifa ya mahakama.