Wanafunzi watumia Uji kutengeneza Pombe

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mpango wa kuwalisha wanafunzi shuleni

Gazeti moja nchini Afrika Kusini, limechapisha ripoti kuwa baadhi ya wanafunzi katika shule kadhaa nchini Zimbabwe wanatumia uji kutengeneza pombe.

Kufuatia taarifa hiyo, shule za bweni nchini humo zimepiga marufuku wanafunzi wao kutoleta vyakula shuleni.

Wazazi sasa wameonywa kuwa wanafunzi wanaorejea shuleni kwa muhula mpya, watapokonywa vyakula walivyobeba kwa sababu baadhi yao wanachanganya chakula hicho na sukari pamoja na Hamira au Chachu na Kuacha chakula hicho kipigwe na jua na kisha kugeuka kuwa pombe.