Mkuu wa Majeshi anusurika jaribio la mauaji

Image caption Prime Niyongabo

Mkuu wa majeshi nchini Burundi, Generali, Prime Niyongabo, amenusurika jaribio la mauaji mapema hii leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Bujumbura.

Walioshuhudia shambulio hilo wamesema msafara wa Mkuu huyo wa Majeshi, ulishambuliwa na watu wasiojulikana kwa gruneti and makomboa, wakati alipokuwa akielekea ofisini.

Ripoti zinasema watu saba waliuawa kweney shambulio hilo.

Naibu mkuu wa polisi nchini humo Generali Godefroid Bizimana, walinzi wanne wa Generali Niyongabo na afisa mmoja wa kike wa polisi waliuawa.

Polisi pia imethibitisha kuwa watu wengine wawili waliokuwa miongoni mwa genge lililofanya shambulio waliuawa na mwingine kukamatwa na kwa sasa anahojiwa na maafisa wa polisi mjini Bujumbura.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Burundi

Generali Niyongabo alipata sifa kote duniani kwa kukataa jeshi la nchi hiyo kugawanywa kwa misingi ya kisiasa wakati wa mzozo wa kisiasa uliokumbwa taifa hilo, wakati wa maandamano ya kupinga uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula wa tatu.

Tangu kuapishwa na rais Nkurunziza kwa muhula wa tatu, idadi ya watu mashuhuri waliouawa nchini humo imekuwa ikiongezeka kila uchao, licha ya ahadi ya rais Pierre Nkurunziza kuwa atawapokonya waasi wote silaha.