Ethiopia kukaribsiha mwaka wa 2008 kesho

Image caption Wachuuzi wa maua hasa zile za kitamaduni kwa kuukaribisha mwaka mpya maarufu kama adey abeba

Raia wa Ethiopia wanajianda kwa sherehe za mwaka mpya hii kesho kuukaribishwa mwaka wa 2008.

Kalenda ya Ethiopia ni miaka saba ya Kalenda zinazotumika kote duniani.

Barabara za miji, maduka na hata makaazi ya watu zimepamba vilivyo kwa maua na taa za kumetameta.

Wafanyabiashara nao wamenufaika pakubwa huku raia wakinunua bidhaa mbali mbali katika harakati za kusherehekea mwaka mpya.

Image caption Nyasi za kutundika sakafuni wakati wa sherehe za mwaka mpya

Wachuuzi wa maua hasa zile za kitamaduni kwa kuukaribisha mwaka mpya maarufu kama adey abeba, wamepata biashara ya hali ya juu.

Kwa sasa fundu moja la maua hiyo inauzwa kwa Birr 10 pesa za Ethiopia ambazo ni sawa na dola 0.50.

Pia nyasi zinazotundikwa sakafuni wakati wa sherehe hizo zimepata wateja wengi.