Mvua yasimamisha mechi za US Open

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Serena Williams

Michuano ya US Open kwa upande wa kinadada imesimamishwa kwa muda baada ya mvua kali kunyesha hali iliyosababisha ugumu wa mchezo huo. Serena Williams atapaswa kusubiri mpaka ijumaa ya leo kuendelea na ratiba ya kalenda ya Grand slam ya nusu fainali kwa wanawake ambapo atacheza dhidi ya Roberta Vinci. Hali hiyo ya mvua haikuzuia mchezo wa wanaume na uliendelea kama ulivyopangwa ambapo matumaini ya bara la Afrika kuendelea kuwepo katika michuano hiyo yalifikia tamati baada ya Kevin Anderson wa Afrika Kusini kushindwa kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali kwa kufungwa na Stan Wawrinka seti 6-4 6-4 6-0.

Hivyo kwa wanaume nusu fainali itakuwa:

Roger Federer vs Stan Wawrinka.

Novak Djokovic vs Marin Cilic.