IOC yajadili wakimbizi wa Syria

Kambi ya wakimbizi kutoka Syria nchini Jordan Haki miliki ya picha Reuters

Jumuia ya Nchi za Kiislamu (Organisation of Islamic Cooperation) inafanya mkutano wa dharura Jumapili mjini Jeddah, Saudi Arabia, kujadili msukosuko kuhusu wakimbizi.

Nchi zanachama, (Jordan, Uturuki na Libnan) zina wakimbizi milioni nne waliohama makwao kwa sababu ya vita lakini malalamiko yanazidi kuhusu mchango wa Saudi Arabia na mataifa ya Ghuba.

Ijumaa, maafisa wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Saudi Arabia walisema nchi hiyo ina Wasyria milioni mbili lakini waandishi wa habari wanasema kuna shaka kubwa kuhusu idadi hiyo.

Umoja wa Mataifa unasema msaada zaidi unahitajika sana kwa ajili ya wakimbizi kutoka Syria waliopata hifadhi katika nchi jirani.