Pande hasimu zakubaliana Libya

Haki miliki ya picha getty
Image caption Libya

Mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Libya anasema kuwa wawakilishi wa serikali mbili zinazozana nchini humo wameafikia makubaliano ya kisiasa.

Hatahivyo maelezo kuhusu makubaliano hayo yalioafikiwa katika mazungumzo nchini Morocco hayajulikani na kwamba hayatahitaji kuidhinishwa na mabunge mawili ya taifa hilo.

Lakini umoja wa mataifa una matumaini kwamba makubaliano ya mwisho yatatiwa saini wiki ijayo.

Mwandishi wa BBC katika eneo la kaskazini mwa Afrika anasema kuwa Libya inaonekana kumaliza tofauti zake.

Lakini amesema kuwa wapiganaji walio na uwezo mkubwa wa kijeshi hawajawakilishwa katika mazungumzo hayo na kwamba makubaliano yoyote yalioafikiwa bila wao yatakuwa vigumu kuidhinisha.