Wakimbizi 4000 waingia nchini Hungary

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi

Idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wanaripotiwa kuingia nchini Hungary siku ya Jumamosi

Zaidi ya watu 4000 walitembea na kuvuka mpaka na serbia wakati ambapo utawala nchini Hungary unakamilisha mipango ya kufunga mpaka wake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Polisi wa Hungary

Hungary imeweka ua mwembamba na kutuma jeshi kusaidia polisi kufuata agizo lililotolewa na waziri mkuu wa nchi hiyo Victor Oban ambalo litaanza kutekelezwa siku ya jumanne.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi walioingia Hungary

Awali Hungary ilimuita balozi wa Austria kutokana na mzozo uliopo kati ya nchi hizo baada ya Chansela wa Austria Werner Faymann kufananisha vitendo vya Hungary dhidi ya wahamiaji sawa na jinsi utawala wa Nazi nchini Ujerumani ulivyowatendea wayahudi.