Viwango vya juu vya joto vitakumba Dunia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viwango vya juu vya joto vitakumba Dunia

Miaka miwili inayokuja itakuwa nyenye viwango vya juu zaidi vya joto kote duniani kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Uingereza.

Ofisi hiyo inaonya kuwa kutashuhudiwa mabadiliko makubwa huku gesi chafu zikitarajiwa kwa na athari katika mabadiliko ya hali ya hewa.

Kulingana utafti uliofanywa, unaonyesha kuwa msimu wa El Nino kwa unashuhudiwa eneo la Pacific unatarajiwa kusambaa kote duniani.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Gesi chafu huchangia mabadiliko ya hali ya hewa

Uchunguzi huo pia unaonyesha kuwa msimu wa joto barani ulaya huenda ukawa wenye kibaridi kwa muda wakati sehemu zingine za dunia zitakaposhuudia kupanda kwa viwango vya joto.

Mkurugenzi wa idara utabiri wa hali ya hewa nchini Uingereza Prof Stephen Belcher, anasema , inaeleweka kuwa masuala ya asili huchangia kubadilika kwa hali ya hewa kila mwaka lakini viwango vya juu vya joto vya mwaka huu, ni ishata ya athari zinazochangiwa na kuongeza kwa gesi chafu duniani.