Dada Dj mkenya ashinda tuzo la Nollywood

Image caption DJ Pierra Makena

Mwanadada Dj kutoka nchini Kenya Pierra Makena ametunikiwa tuzo kama mcheza filamu bora kwa kushiriki katika filamu moja ya kinigeria ya "When Love Comes Around," wakati wa awamu ya tano ya tuzo za Nollywood ambazo pia zinafahamika kwa tuzo za Oscar za Afrika.

Dj huyo anayeendesha mambo yake kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi, anasema alishangazwa na tuzo hilo licha ya yeye kuwa maarufu katika nyanja ya muziki tu.

Image caption DJ Pierra Makena

Makena ambaye alikuwa akiigiza kama, Didi the unlucky, ambaye ni mwanamke aliye na hamu ya kupendwa, alitangazwa kuwa mshindi kwenye sherehe zilizoandaliwa katika ukumbi wa Orpheum, jimbo la California nchini Marekani mnamo tarehe 12 mwezi huu.

Makena alielezea furaha yake baada ya ushindi huo na kuandika kwenyr mtandao wa Instagram akisema kuwa, Mabibi na Mabwana, Nimeshinda! Nimeshinda! Nimeshinda!