Jerusalem wakumbwa na machafuko

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jerusalem wakumbwa na machafuko

Leo ni siku ya pili ya makabiliano katika eneo la al-Aqsa mjini Jerusalem, kati ya polisi wa Israeli na vijana wa Kipalestina wenye hamaki.

Idara ya Polisi inasema kuwa, vijana waliofunika nyuso zao, wanawashambulia kwa mawe kabla ya kukimbilia misikitini.

Hali hiyo inakuwa vigumu kwa polisi kuvamia eneo hilo kwani ni takatifu kwa waislamu na wayahudi.