Kwa nini nchi za Kiarabu haziwachukui wakimbizi wa Syria

Haki miliki ya picha .
Image caption Wakimbizi wa Syria

Picha za wakimbizi wa Syria waliokwama katika mipaka na vile vile katika vituo vya treni bila kutaja picha ya mvulana mdogo wa miaka mitatu Alan Kurdi aliyekuwa amesombwa na maji katika ufukwe wa bahari wa Uturuki zimezua hisia kwa juhudi zaidi kuchukuliwa ili kuwasaidia wale wanaotoroka vita.

Hasira zaidi zimelenga mataifa ya uarabuni kama vile Saudi Arabia,Bahrain,Kuwait,Qatar,Oman na UAE ambao wamefunga milango yao kwa wakimbizi hao.

Kufuatia ukosoaji huo,ni muhimu kukumbuka kwamba mataifa hayo ya Uarabuni hayajataka kuwasaidia wakimbizi wa Syria.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption viongozi wa Uarabuni

Ukarimu wa watu binafsi umewasaidia pakubwa wakimbizi hao.

Kampuni za kibinfasi za wahisani zimechangisha maelefu ya madola na wakati wafanyikazi wa viwanda vya kitaifa kwa mfano kile cha mafuta cha Qatar,walipoulizwa iwapo wako tayari kutenga kiwango fulani cha fedha kila mwezi ili kuwasaidia wakimbizi hao wa Syria ,wengi wao walikubali.

Mataifa ya Uarabuni yametoa takriban dola milioni 900 kupitia kampuni za wahisani pamoja na michango ya watu binafsi.

Hatahivyo,huku vita vya Syria vikiendelea ,imekuwa vigumu kuwatafutia raslimali wakimbizi hao wanaoishi katika kambi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wakimbizi wa Syria

Ulimwengu umelazimika kutafuta suluhu nyengine ili kukabiliana na idadi kubwa ya wakimbizi hao,kwa kuwa raia hao wa Syria wamechoshwa na vita na kuishi katika kambi bila matumaini ya kijamii na fedha wamelazimika kuondoka maeneo hayo ya vita ili kutafuta maisha bora ya baadaye.

Kwa ufupi,utoaji wa chakula na maji kwa watu wanaoishi katika kambi ilikuwa suluhu kwa tatizo la jana.

Swala tata zaidi ni kuwatafutia mamia ya maelfu ya watu mahala pa kuishi,na ni hapo ambapo mataifa ya Uarabuni yameshindwa kutafuta jibu.

Huku mataifa hayo ya Uarabuni yakiwa yamewaruhusu baadhi ya raia wa Syria, Saudi Arabia inasema kuwa imechukua zaidi ya raia laki tano tangu mwaka 2011,wakiwa wafanyikazi wahamiaji lakini hakujakuwa na sera yoyote kwa mataifa hayo kuwatafutia hifadhi wakimbizi wanaowasili kwa wingi bila wadhamini ama hata vibali vya kufanya kazi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wakimbiz wa Syria

Ili kujaribu kuelezea hili,utahitaji kuingia ndani zaidi ili kubaini hofu ya mataifa hayo ya Uarabuni kuhusu uthabiti wa kisiasa katika mipaka yao pamoja na maswala makubwa ya vitambulisho na dhana kuhusu umuhimu wa kuwa raia wa Uarabuni.

Mnamo mwaka 2012,wakati vita vya Bashar Al Asaad vilipoanza na kubainisha ushindani mkubwa kati ya mataifa ya Uarabuni yenye wasunni na washirika wao wa Iran,hofu ilianza kuyatawala mataifa hayo kwamba raia wa Syria wanaomtii rais Assad watalazimika kuingia mataifa hayo ya Uarabuni ili kulipiza kisasi.

Ukaguzi wa wakimbizi wa Syria wanaoelekea katika mataifa hayo ya Uarabuni ulianza na ilikuwa vigumu kwa raia wa Syria kupokea vibali vya kufanya kazi ama hata kuvipiga chapa mpya ili kuendelea kufanya kazi.

Sera hiyo haijabadilishwa nchini Qatar,Saudi Arabia ama hata UAE kwa hofu ya uwezekano wa raia walio watiifu kwa rais Assad kulipiza kisasi.

Uvumi umeendelea kuwepo katika mataifa hayo ya kiarabu kwa kipindi cha miaka mitatu kuhusu seli za magaidi wanaokamatwa na kuzuiliwa ijapokuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa mpango wa wafuasi wa Assad ambao umeripotiwa.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mataifa mengi ya Uarabuni wanahofu kwamba raia wanaomtii Bashar al Asaas huenda wakalipiza kisasi

Idadi ya maelfu ya raia wa Syria wanaotaka kuingia katika mataifa hayo huenda ikaathiri uchumi unaotegemewa na mataifa hayo ili kuweza kufanya kazi.

Kwa mfano,idadi ya raia wa UAE na Qatar iko chini kwa asilimia 10 ya raia wa mataifa hayo.

Idadi kubwa ya raia ni wafanyikazi wanaofanya kazi katika eneo moja hadi jingine.

Wageni huruhusiwa pekee iwapo wake zao ama waume zao wana kazi kamili,hauwezi kusalia katika mataifa hayo ya Uarabuni bila kazi na wakati kandarasi zao zinapokamilika basi wahamiaji wote hulazimika kurudi makwao.

Hivi ndivyo mataifa hayo ya Urabuni yanavyofanya kazi.Kwa hivyo wazo la maelfu ya wageni wanaoingia bila kazi ama bila siku rasmi ya kurudi makwao huyaweka mataifa hayo kati hali isiyo nzuri.