Hotuba ya Mugabe yakumbwa na upinzani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mugabe

Bunge la Zimbabwe limeahirisha matangazo ya hotuba ya rais Robert Mugabe baada ya upinzani kutishia kuvuruga hotuba hiyo.

Mwezi uliopita ,wakati wa hotuba yake kwa bunge la taifa hilo,wanachama wa upinzani walimzoma kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 91.

Wanamlaumu kwa kudorora kwa uchumi wa taifa hilo.

Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.