Ushahidi dhidi ya Ntaganda watolewa ICC

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bosco Ntaganda

Shahidi wa kwanza ameanza kutoa ushahidi wake katika kesi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Congo Bosco Ntaganda katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita mjini The Hague.

Bwana Ntaganda anakabiliwa na mashtaka ikiwemo mauaji,ubakaji na kusajili wanajeshi watoto mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo muongo mmoja uliopita.

Shahidi huyo aliyetoa ushahidi nyuma ya pazia ili asitambuliwe amesema kuwa wanajeshi waasi waliwasili katika kijiji anachoishi na kuiba pesa,mbali na kuharibu nyumba yake.

Haki miliki ya picha
Image caption Bosco Ntaganda

Bwana Ntaganda amekana zaidi ya mashtaka 18 dhidi yake.

Mashtaka hayo yanahusishwa na mizozo katika mkoa wa Ituri mnamo mwaka 2002 na 2003.