Mugabe asoma hotuba ya zamani kimakosa

Robert Mugabe Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi huyo alitarajiwa kusoma hotuba sahihi baadaye hotelini

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe alisoma hotuba isiyofaa kimakosa wakati wa kufunguliwa kwa bunge la nchi hiyo Jumanne.

Hotuba aliyoisoma ndiyo ile ile aliyoitoa akihutubia taifa Agosti 25, alipozomewa na wabunge wa upinzani.

Msemaji wake aliambia gazeti la serikali la Herald kwamba kosa hilo lilitokana na suitafahamu katika afisi ya katibu wake.

Msemaji wa rais huyo George Charamba aliomba radhi kwa kosa hilo na kuongeza kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 91 angesoma hotuba sahihi baadaye hotelini Harare.

Wakati wa kusomwa kwa hotuba, wabunge wa chama cha upinzani cha MDC ambao awali ilihofiwa wangevuruga hotuba hiyo walikaa kimya.