Mwindaji atuhumiwa kusafirisha swara

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwindaji mashuhuri ,theo Bronkhrost

Mtaalamu wa uwindaji anayeshutumiwa kuhusika na kifo cha simba aliyepewa jina Cecil nchini Zimbabwe amekamatwa kwa tuhuma za kusafirisha swara 29 kimagendo nchini Afrika Kusini.

Theo Bronkhorst anazuiliwa mjini Bulawayo polisi wa nchini humo wamethibitisha.

Bwana huyo yuko nje kwa dhamana ya kesi inayomkabili ya kumuua Simba bila ya kuwa na vibali mwezi wa saba na hivyo kuhitimisha kazi yake daktari wa meno Marekani Walter Palmer

Kesi hi imesababisha kilio cha kimataifa hadi daktari Palmer kukimbilia mafichoni kwa miezi kadhaa na kurudi kazini hivi karibuni.

Wahifadhi nchini Zimbabwe wamesema Cecil alikuwa kivutio kikubwa cha watalii. Kabla ya kutoka kwenye hifadhi ya taifa nchini humo simba huyo aliwekewa mtego uliomfanya atoke nje na kupigwa risasi.

Bronkhorst anatarajiwa kusimamishwa kizimbani siku ya Jumatano kwa kosa kusafirisha swara 29 kwa magendo.

Watu wengine watatu raia wa Afrika Kusini wamekamatwa pia kwa kusafirisha swara hao. Watu hao walikamatwa baada ya gari lao kukwama mtoni.