Lori la mafuta lawauwa watu 170 Sudan K

Haki miliki ya picha
Image caption Sudan Kusini

Takriban watu 170 wameuawa baada ya lori la mafuta kulipuka Sudan Kusini kulingana na msemaji wa rais.

Lori hilo lilikosa mwelekeo na kutoka kando ya barabara katika eneo la Maridi,magharibi mwa jimbo la Equitorial kabla ya raia kuanza kufyonza mafuta wakati lilipolipuka alisema Ateny Wek Ateny.

Takriban watu 59 wanadaiwa kujeruhiwa.

Hospitali katika eneo hilo zimezidiwa majeruhi na maafisa wa serikali wameliomba shirika la msalaba mwekundu na umoja wa mataifa kutoa usaidizi.

Lori hilo lilikuwa likisafiri kutoka mji mkuu Juba kelekea Maridi,umbali wa kilomita 250 lilipokosa mwelekeo.

Wakaazi wa jamii zilizopo karibu walifanya kama wanavyofanya raia wengine Afrika kwa kufyonza mafuta kabla ya kupotea.

Waziri wa habari nchini humo Charles Kisagna ameiambia Reuters anahofu kuhusu wale waliojeruhiwa.