Croatia yawaruhusu wahamiaji kuingia Hungary

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri Mkuu wa Coatia, Zoran Milanovic, anasema nchi yake itaendelea kuwaelekeza wakimbizi waelekee Hungary.

Waziri Mkuu wa Coatia, Zoran Milanovic, anasema nchi yake itaendelea kuwaelekeza wakimbizi waende Hungary.

Alisema hakuna makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Hungary.

Hata hivyo rais huyo alisema Croatia itailazimisha Hungary kuwapokea wakimbizi hao.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Hungary imemlaumu Croatia kwa kushiriki katika ulanguzi wa watu

Hungary imeishutumu Croatia, kuwa inavunja sheria ya kimataifa, kwa kuwapeleka wahamiaji moja-kwa-moja kwenye mpaka wake, bila ya kuwa-a-ndikisha kwanza.

Wahamiaji na wakimbizi kama elfu 17, (17,000) wameingia Croatia tangu Jumatano, wakitaraji kufika Ujerumani na nchi nyengine za Ulaya Kaskazini.

Hungary imemlaumu Croatia kwa kushiriki katika ulanguzi wa watu, baada ya utawala nchini Croatia kuanza kusafirisha wahamiaji kwenda nchini Hungary bila kuwaandikisha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wahamiaji na wakimbizi 17,000 wameingia Croatia tangu Jumatano

Akiongea na BBC waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Croatia Vesna Pusic, ametaka kuwepo hatua za pamoja kutatua suala hilo na kujumuisha nchi zote za ulaya.