Misri yaapisha serikali mpya

Image caption Waziri wa zamani wa mafuta, nchini Misri, Sherif Isma'il, ameapishwa kuongoza serikali mpya nchini humo

Serikali mpya ya Misri imeundwa, juma moja baada ya ile iliyopita kujiuzulu, kwa sababu ya kashfa ya rushwa.

Rais Abdel Fattah al-Sisi, amemuapisha waziri wa zamani wa mafuta, Sherif Isma'il, kuwa waziri wake mkuu.

Mawaziri kadha muhimu, kama wa fedha, mambo ya ndani ya nchi, na mashauri ya nchi za nje, hawakubadi-lishwa.

Serikali mpya ya Misri inakabiliwa na changamoto chungu nzima, baada ya miaka kadhaa ya machafuko ya kisiasa.

Inahitaji sana kuvutia uwekezaji kutoka nchi za nje.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Serikali hiyo inakabiliwa na changamoto ya usalama huku wapiganaji wa makundi ya kigaidi wakizidisha mashambulizi dhidi ya jeshi

Aidha Misri inahitaji uwekezaji mkubwa ilikugharimia sekta ya mafuta.

Pia usalama umeanza kudorora huku wapiganaji wa makundi ya kigaidi wakizidisha mashambulizi dhidi ya jeshi, hasa katika jimbo la Sinai.