Marekani yailegezea Cuba vikwazo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Bendera za marekani na Cuba

Rais wa Marekani Barack Obama amezungumza na mwenzake wa Cuba Raul Castro kwa njia ya simu, muda mfupi baada ya marekani kutangaza kuwa imelegeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya kisiwa hicho.

Kuanzia siku ya Jumatatu makampuni fulani nchini Marekai kwa mara ya kwanza yataanza kufanya ushirikiano na makampuni ya Cuba na kufungua ofisi nchini humo.

Vikwazo vya usafiri pia navyo vimelegezwa kwa raia wa marekani.

Rais Castro amezungumzia haja ya kuondolewa kwa vikwazo vyote, lakini bado hajasema ikiwa ataruhusu makampuni ya Marekani kama Mcdonalds na Starbucks kufungua biashara nchini Cuba.