Dalili za mapatano Burkina Faso

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Dalili za mapatano Burkina Faso

Wapatanishi wa Afrika wanasema kuwa wanakaribia kumaliza mapinduzi ya kijeshi nchini Burkina Faso.

Viongozi hao wa mataifa ya Afrika Magharibi wanasema kuwa mazungumzo yao yanalenga kurejeshwa kwa utawala wa kiraia wa mpwito.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kuna uwezekano mkubwa kuwa viongozi wa wa mapinduzi hayo wako tayari kumuachilia rais Michel Kafando kutoka kizuizi cha nyumbani

Rais wa Benin, Yayi Bon, anasema kwa kuna uwezekano mkubwa kuwa viongozi wa wa mapinduzi hayo wako tayari kumuachilia rais Michel Kafando kutoka kizuizi cha nyumbani na kumrudish mamlakani.

Mazungumzo yamekuwa yakifanyika katika mji mkuu Ouagadougou baada ya siku ya tatu ya maandamano ya kupinga mapinduzi ya rais Kafando yaliyofanywa na kikosi cha kumlinda rais.

Akiongea na kiongozi wa mapinduzi hayo, jenerali Gilbert Diendere, rais wa Benin anasema kuwa anatarajia kile alichokitaja kuwa habari njema kutangazwa baadaye leo Jumapili.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu kumi wamepoteza maisha yao huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa

Watu kumi wamepoteza maisha yao huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa katika makabiliano baina ya vyombo vya usalama na waandamanaji waliopinga mapinduzi hayo ya Alhamisi.

Image caption Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya Gilbert Diendere atatoa masharti yepi

Waandamanaji wanamtaka rais wa kipindi cha mpwito Kafondo kuendelea kushikilia hatamu hadi pale uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba utakapomalizika.

Haijabainika hadi kufikia sasa kiongozi wa mapinduzi haya atatoa masharti yepi ya kurejesha mamalaka kwa rais Kafondo na utawala wake.