Uchaguzi ni leo Ugiriki

Image caption Uchaguzi ni leo Ugiriki

Watu nchini Ugiriki wanaelekea kwa vituo vya kupigia kura, kwenye uchaguzi mwingine mkuu ambao ni wa tano ndani ya kipindi cha miaka sita.

Kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Syriza ambaye ni waziri mkuu wa zamani Alexis Tsipras aliitisha uchaguzi huo baada ya kupoteza ushawishi wake bungeni mwezi uliopita.

Umaarufu wa bwana Tsipras ulishuka baada ya kutia sahihi mpango mpya na viongozi wa ulaya , ili nchi yake ipewe msaada.

Kura ya maoni unaonyesha kuwa uchaguzi huo ni kinyanganyiro kati ya chama cha Syriza na kile cha New Democracy.