Ni rasmi sasa Museveni kuiwakilisha NRM

Image caption Besigye sasa atapambana na rais Yoweri Museveni, kwa mara ya nne

Hatimaye Rais Yoweri Museveni wa Uganda amepokea rasmi tikiti ya kuwa uwakilishi wa chama tawala NRM katika uchaguzi mkuu ujao.

Museveni alipokea rasmi tikiti hiyo katika hafla iliyohudhuriwa na kamati kuu ya chama hicho mjini Kampala.

Image caption Wafuasi wa Museveni

Museveni alitumia fursa ya hiyo ya kuwapiga vijembe wapinzani wake kwa kusema kuwa chama cha national resistance Movement sio chama limbukeni katika siasa za Uganda.

''NRM ni chama ambayo imepikwa ikapikika ikipitia katika hali ngumu na pia katika mafanikio''

'NRM imepitia tanuri ya historia ya Uganda.'

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Besigye sasa atapambana na rais Yoweri Museveni, kwa mara ya nne

Hiki ndicho chama kitakachoikomboa Uganda''Alisema Museveni kupitia kwa mtandao wake wa Twitter.

Rais Museveni atakuwa anawania muhula wa tano licha ya upinzani kudai kuwa muda wake umemalizika.

Museveni sasa atakabiliania na kiongozi wa upinzani , Kizza Besigye, na aliyekuwa waziri mkuu Patrick Amama Mbabazi .

Besigye sasa atapambana na rais Yoweri Museveni, kwa mara ya nne katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuandaliwa mwaka ujao.

Besigye alishinda uteuzi wa chama kikuu cha upinzani FDC.

Alikuwa akiwania tikiti hiyo dhidi ya Mugisha Muntu.

Kwa upande wake John Patrick Amama Mbabazi ambaye alikuwa waziri mkuu wa zamani wa Uganda na mshirika wa karibu sana wa miaka mingi wa rais Museveni anagombea kiti hicho cha urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2016 kama mwakilishi wa kujitegemea.

Image caption Waziri mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi

Pia mwingine aliechukua fomu za uteuzi ni Prof Baryamureeba zamani akihudumu kama makamu mkuu wa chuo kikuu cha Makerere.