Pistorius kujua hatima yake baada ya wiki 2

Image caption Oscar Pistorius kusubiri gerezani kwa majuma mawili zaidi

Kamati maalum ya kutoa msamaha imeahirisha kwa majuma mawili kauli ya iwapo mwanariadha Oscar Pistorius aliyepatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mpenzi wake,anastahili msamaha na kuwachiliwa huru au la.

Msemaji wa idara ya magereza Manelisi Wolela,amenukuliwa akisema kuwa jopo hilo liliahirisha kikao kitakachotoa kauli hiyo baada ya kukutana mjini Durban Afrika Kusini.

''Jopo hili lilikuwa linashughuli zingine zilizopewa kipao mbele na hivyo halikuweza kujadili swala la Pistorius.''

''kikao kitakachofuatia kitakuwa baada ya majuma mawili nafkiri wakati huo ndio tutaweza kujua iwapo swala la Oscar Pistorius litajadiliwa au la.''alisema Manelisi Wolela

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Upande wa mashtaka umekata rufaa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia kwa nia ya kumfunga kwa mika 15 jela

Vikao hivyo vinatarajiwa kubaini iwapo Pistorius aliyehukukumiwa kifungo cha miaka 5 gerezani atawachiliwa huru ama aendelee kutumikia kifungo cha miaka 5 jela.

Hata akiwachiliwa huru, Oscar Pistorius huenda akajipata amerejea gerezani tena kwani upande wa mashtaka umekata rufaa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia

Waziri wa haki nchini humo, alizuia mwanariadha huyo kuachiliwa huru mwezi uliopita kama ilivyokuwa imetarajiwa.

Mahakama nchini humo ilimpata Pistorius na hatia ya kuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka wa 2013.

Pistorius alimpigia risasi Steenkamp akiwa bafuni nyumbani kwake mjini Pretoria, baada ya kumshuku kuwa ni mwizi.

Haki miliki ya picha AFP Getty
Image caption Pistorius alimpigia risasi Steenkamp akiwa bafuni nyumbani kwake mjini Pretoria, baada ya kumshuku kuwa ni mwizi.

Upande wa mashtaka umekataa rufaa ya hukumu hiyo ukisema kuwa Pistorius anapaswa kuhukumiwa kwa mauaji.

Chini ya sheria za Afrika Kusini,mtu anaweza kusamehewa mradi ametumikia sehemu moja juu ya 6 ya kifungo chake gerezani na awe na nidhamu njema.

Mawakili wa Pistorius wanatarajiwa kuwasilisha nyaraka zao kupinga rufaa hiyo.