Apple wavamiwa kimitandao

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kampuni ya Apple ya nchini Marekani.

Kampuni ya Apple ya Marekani imesema kuwa ipo katika hatua za kukabiliana na shambulio la kimitandao,ambapo wamebaini kuwa program hatari ya kimitandao iliyopo kwa watumiaji wa simu za IPhone na iPad nchini China.

Watalaam wa ndani ya kampuni hiyo wamesema kuwa inaelezwa kuwa hili ni moja la shambulio kubwa la kimitandao kuwahi kuikumba kampuni hiyo.

Apple wanasema kwua wavamizi hao wa kimitandao wanasema wamebuni namba za siri ambazo huwawezesha watumiaji wa vifaa hivyo vya Apple kuingiziwa programu zinazoathiri mawasiliano yao.

Msemaji wa Apple anasema kuwa kampuni yao imeondoa kwenye mzunguko wa soko vifaa vyote vinavyotiliwa shaka kuingiliwa na wavamizi hao wa kimitandao nchini China.