Waislamu washerehekea sikukuu ya Eid

Eid al-Adha
Image caption Sikukuu ya Eid al Adha ni moja ya sikukuu mbili za Eid katika dini ya Kiislamu

Waumini wa dini ya Kiislamu wamesherehekea siku ya Eid al-Adha katika mataifa tofauti kwa kuungana na jamaa ndugu na marafiki katika ibada.

Walianza kujumuika asubuhi misikitiki kwa sala na hotuba kutoka kwa viongozi wa kidini.

Waumini zaidi waliojumuika mjini Makka nchini Saudi Arabia kwa ibada ya hajj wamesherehekea katika mji huo.

Sherehe za Eid al-Adha huhusisha kuchinja mifugo na kugawa nyama kwa watu wasiojiweza katika jamii.

Sherehe hiyo ni moja kati ya mbili za Eid zinazosherehekwa na Waislamu kila mwaka, hiyo nyingine ikiwa Eid ul-Fitri inayosherehekewa baada ya mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhan.

Mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay alipiga picha hii ya watoto katika mji wa Garissa, kaskazini mashariki mwa Kenya.

Image caption Uwanja wa Jenerali Mohamud Eid, Garissa ulijaa waumini

Katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi jana maeneo mengi yalikuwa yamegeuzwa kuwa soko la mifugo waumini wakinunua mifugo wa kuchinjwa leo. Mwandishi wa BBC Ahmed Hassan alipata mbuzi wakiwa kwa wingi.

Image caption Sikukuu ya Eid al Adha, Waislamu huchinja mifugo na kugawia nyama watu wasiojiweza katika jamii

Katika uwanja wa Kiislamu wa Sir Ali, Kilimani, Nairobi hii ndiyo hali aliyokumbana nayo mwandishi wa BBC Seif Abdallah Dzungu leo.