Kujitoa uhai:Vijana wengi wamo hatarini

Image caption Vijana waliobalehe wamekuwa wakijiua kwa wingi katika mataifa yenye mapato ya chini

"Watu hudhani ni uhalifu kujiua, lakini sivyo hivyo, anasema Lauren Ball mwenye umri wa miaka 20 ambaye amejaribu kujiua kwa mara kadhaa.

Mara sita, huku jaribio lake la hivi karibuni likiwa lile la mwaka 2014.

''Najua imekuwa vigumu sana kwa familia yangu'," Ball alikiambia kipindi cha vijana cha BBC Newsbeat.

''Sidhani kama ni kitu ambacho naweza kukisahau, alisema mama huyo mwenye mtoto wa miaka 14 ambaye alijiua miaka miwili iliopita katika mji mmoja uliopo pwani ya mji wa Devon nchini Uingereza.

Jamii nyingi ndio zimeanza kuzungumzia kuhusu afya ya akili. Wengine bado hawazungumzii. Wakati huohuo wataalam wa masuala ya afya wameonya kuwa kuna umuhimu wa kukabiliana na janga la kujitoa uhai miongoni mwa vijana.

Suala ambalo limeonekana kama miko kwa muda mrefu,linasema shirika la afya duniani.

Haki miliki ya picha DIX FAMILY
Image caption Kijana Izzy_Dix

Mbona vijana wadogo wanajiua?

TAKWIMU DUNIANI

Watu 803,900

hujiua kila mwaka – idadi hii ni sawa na mtu mmoja kila sekunde 40

  • Nambari 15 kwa kusababisha vifo katika marika yote

  • Nambari 2 kwa kusababisha vifo kwa vijana (umri 15-29)

"Kujitoa uhai ni suala gumu na huwa hakuna sababu moja ambayo mtu huamua kufanya hivyo''.

Kile kinachojulikana ni kwamba takriban watu 800,000 hufariki kwa kujitoa uhai kila mwaka.

Kulingana na takwimu kutoka shirika la WHO, kuna takriban majaribio 20 kwa kila kisa.

Utafiti wa shirika la afya duniani kuhusu vifo mnamo mwaka 2012 unathibitisha kuwa kujitoa uhai ni janga duniani kote.

Muhimu zaidi ni kwamba tofauti ya kimaisha huwa na athari kubwa miongoni mwa vijana.

Utafiti huo unaonyesha kwamba vifo vya kujitoa uhai hupatikana kwa wingi katika vijana wa umri kati ya 10 hadi 25 katika mataifa yenye mapato ya chini.

VIJANA

Je ni nini husababisha vifo hivi ?

1.3 milioni

Vijana waliobalehe hufariki kila mwaka

duniani kutokana na mambo yanayoweza kuzuiwa

  • 1. Ajali za barabarani ndizo chanzo kikuu cha 11.6% ya vifo

  • 2. Asilimia 7.3 ya vijana hujiua

  • 3. HIV/Ukimwi na magonjwa ya kupumua

  • 4. Vita baina ya vijana

Kulingana na jinsia:Kwa jumla wanaume wengi hufariki kwa kujitoa uhai ukilinganisha na wanaume.

Wasichana hujaribu sana kujiua ukilinganisha na wavulana, lakini wavulana wengi hufanikisha majaribio hayo ikilinganishwa na wasichana, kulingana na Fleischmann.

Katika mataifa tajiri, wanaume wanaofariki kwa kujitoa uhai ni mara tatu ukilinganisha na wanaume, lakini katika mataifa yalio na mapato ya kadri idadi hiyo ni ndogo.

VIWANGO VYA JUU ZAIDI DUNIANI

Vifo kati ya vijana 100,000

1. India

ina vifo 35.5 (taifa pekee ambako wanawake wanaojiua wanazidi wanaume)

  • 2. Zimbabwe 30.9

  • 3. Kazakhstan 30.8

  • 4. Guyana 29.7

  • 5. Suriname 28.2

Takwimu mbaya zaidi zimeonyesha kuwa katika maeneo mengine ya dunia kujitoa uhai kunaongoza miongoni mwa sababu za vifo kwa watu kati ya umri wa mika 15 na 19, hivyo ndio hali ilivyo kusini mashariki mwa Asia.

[an error occurred while processing this directive]

Barani Afrika takwimu hizo ni za uhakika. Idadi ya vifo vinavyotokana na mtu kujiitoa uhai ni watu 9 kwa watu 100,000 ambayo ni idadi ya kiwango cha juu ikilinganishwa na jimbo lolote lile isipokuwa Kusini mashariki mwa Asia ambapo ni watu 25 kwa kila watu 100,000.

Onyo

Wataalam wanasema kuwa kujitoa uhai hakufanyiki tu, huku utafiti ukionyesha kwamba takriban asilimia 90 ya vijana wanaojitoa uhai wana matatizo ya kiakili.

Chanzo cha tatizo hilo huaminika kuwa shinikizo la kiakili, ikiwa ndio tatizo la kwanza, mbali na ghasia ama utumizi wa dawa za kulevya.

La muhimu zaidi ni kwamba washauri wa maafisa wa afya wanaamini kwamba kuna umuhimu wa mipango ya kuweka kinga ambayo inafaa kufadhiliwa na serikali. Kufikia sasa ni mataifa 28 yalio na mipango hiyo ya kitaifa, kulingana na rekodi za WHO.