Upinzani washindwa kuungana Uganda

Haki miliki ya picha
Image caption Aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni huenda akapata afueni baada ya muungano wa upinzani kushindwa kuungana kufuatia mkutano mrefu wa wiki moja ili kukubaliana kuhusu mgombea mmoja katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Mwandishi wa BBC Paience Atuhaire katika mji mkuu wa Kampala amesema kuwa muungano wa vyama vya demokrasia unavileta pamoja vyama vya upinzani na makundi ya kijamii.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kizza Besigye

Ilitarajiwa kuwa ungemchagua Kizza Besigye kutoka chama cha Forum for Democratic Change ama aliyekuwa waziri mkuu Amama Mbabazi.

Mgombea mmoja wa upinzani ina maanisha kwamba kura zitawekwa katika kikapu kimoja ,lakini huku wagombea kadhaa wa upinzania wakioonekana katika kinyanganyiro ,huneda kura zikagawanyika.