Walinda amani wa Afrika Kusini kuadhibiwa

Monusco Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi hao wa Afrika Kusini wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine

Wanajeshi hamsimi wa Afrika Kusini waliokuwa wakihudumu katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) wameagizwa kurejea nyumbani.

Viongozi wa jeshi nchini Afrika Kusini wamesema wanajeshi hao wataadhibiwa kwa kuwa wamekiuka maadili ya utendakazi.

Taifa hilo lina takriban wanajeshi 1,400 wanaohudumu Congo, wakijaribu kusaidia kukomesha vita mashariki mwa DR Congo.

Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kuhatarisha usalama wa wanajeshi wengine wa UN nchini DR Congo.