Waziri Tanzania afariki dunia

Image caption Celina Kombani

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma nchini Tanzania Celina Kombani amefariki dunia.

Waziri Kombani ambaye pia alikuwa ni mbunge wa jimbo la Ulanga mashariki, amefariki jana Septemba 24, wakati akipata matibabu nchini India.

Alizaliwa Juni 19, 1959, na alikuwa mbunge kupitia chama tawala CCM.

Rais Jakaya Kikwete ni miongoni wa waliotuma risala za rambirambi kumuomboleza waziri huyo.

"Ndugu yetu na mtumishi wa wananchi, Bi Celina Kombani ametangulia mbele za haki. Moyo wangu uko pamoja na familia yake wakati huu wa majonzi," amesema kupitia akaunti yake ya Twitter.