Kituo cha polisi chashambuliwa Nigeria

Haki miliki ya picha bb
Image caption Kituo cha polisi nchini Nigeria chashambuliwa

Watu wenye silaha wameshambulia afisi za kikosi cha siri cha polisi katika mji mkuu wa jimbo la Kogi wa Lokoja nchini Nigeria.

Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji wa risasi ulitokea usiku kucha.

Haijulikani washambuliaji hao walikuwa ni akina nani lakini kumekuwa na majaribio mara kadhaa ya kuwakomboa watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram ambao wanazuiwa katika vituo vya siri vya polisi mjini Lokoja.

Kamishna wa polisi katika eneo hilo amesema kuwa kulikuwa na makabiliano ya risasi pamoja na milipuko.

Amesema kuwa polisi mmoja na wapiganaji watatu walifariki.Amewataja washambuliaji hao kuwa wahalifu.

Hapo awali kumekuwa na majaribio kadhaa kuwaachilia wanachama wa kundi la Boko Haram ambao wanazuiliwa katika kituo kimoja cha siri cha polisi huko Lokoja.